GET /api/v0.1/hansard/entries/953774/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 953774,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/953774/?format=api",
"text_counter": 137,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Madzayo",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 679,
"legal_name": "Stewart Mwachiru Shadrack Madzayo",
"slug": "stewart-mwachiru-shadrack-madzayo"
},
"content": ". Ukumbi huu wa watu waliobobea utakua mjadala wa kila mtu katika kaunti. Hakuna hata mtu mmoja atayekuwa na uwezo wa kumfuta jina la mtu fulani ambaye kamati mzima imemkubali. Itakuwa ni kamati na itakapopitisha, ndivyo vile viongozi wa kaunti ile watafuata. Bw. Naibu Spika, nasisitiza ya kwamba wanaofahamu historia ya Mijikenda ni watu wachache sana. Watu kama sisi tulikuwa na wazee wetu ambao walitueleza vile kulikuwa, lakini hawakuandika historia yetu. Hawakuchukua hiyo habari kutoka kwa mababu zao. Baba yangu angekuwa ameipata historia hiyo kutoka kwa babu yangu. Leo hii ingekuwa akitafakari na kusema: “Mjukuu wangu, kulikuwa hivi au vile.” Naye baba yangu awaambie wajukuu wake: “kutakuwa hivi na vile.” Sisi kama Mijikenda tulikosa hayo yote. Tukiulizwa ni kwa nini tunaitwa Mijikenda au kitabu chetu kiko wapi, hatuwezi sema. Tunaweza kukumbuka vigango vilivyochukiliwa na wazungu na kuturudishia baada ya kutuonea huruma. Kigango ni kile kitu ambacho kinatumika wakati wazee wameketi jioni baada ya watu kuota ndoto mbaya ama kuwa wabaya. Wazee hukaa na kuongea, kumwaga pombe ya mnazi na maji kidogo na kuwaambia watu wasirudie kuwasumbua. Tuonaona wakifanya mambo haya lakini hakuna mahali popote ambapo historia hiyo imeandikwa ilhali ni muhimu. Ukiangalia wale waliopigania Uhuru, wengi wanasema kuhusu Mekatilili wa Menza. Ni kitabu kipi Mekatikili alichokiandika? Wale waliokuwa wanafuatana naye waliandika wapi ile historia? Hakuna. Tunaeleza kwa mdomo tu kwa vizazi vile kwamba tulikua na Mekatilili wa Menza, Mepoho, Ronald Gideon Ngala na Chokwe. Bw. Chokwe ndiye aliyekuwa Spika wa kwanza baada ya Kenya kupata Uhuru. Hivi leo, hatuwezi tukapata historia ya mzee Muinga Chokwe. Ni sisi ambao tumekuja hapa ndio tunaweza kungundua ya kwamba mtu wa kutoka kule nyumbani ndiye alikuwa mtu wa kwanza kuwa Spika na tunajua hayo tukienda katika maktaba. Yeye ndiye aliongoza Bunge ya Kenya tulipopata Uhuru. Hiyo ni jambo ambalo tungejivunia sana lakini historia hiyo haikuandikwa popote. Lazima serikali ya mashinani itengeneze ukumbi ambapo itatambua watu ambao walifanya mambo makubwa na wale ambao walibobea katika mambo ambayo walifanya. Naunga mkono Mswada huu. Ningependa kuona mhe. Rais akiweka kidole chake ili Mswada huu uwe sheria. Hiyo sheria itawafanya viongozi wa kaunti watenge pesa ya kujenga ukumbi mkubwa. Wanakamati wataketi katika huo ukumbi. Ndani ya ukumbi huo kutakuwa na picha ya wale watu ambao waliketi pale ili historia iweze kukumbuka waliotangulia wakaenda mbele za haki. Kama vile wahenga husema."
}