GET /api/v0.1/hansard/entries/953980/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 953980,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/953980/?format=api",
"text_counter": 90,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Faki",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13211,
"legal_name": "Mohamed Faki Mwinyihaji",
"slug": "mohamed-faki-mwinyihaji-2"
},
"content": "Pili, jana asubuhi tulizuru Gereza la Kitui tukiwa na Maseneta wa Kamati ya Haki, Sheria na Haki za Binadamu na Kamati ya Usalama wa Nchi, Ulinzi na Uhusiano wa Kimataifa. Tulipata kwamba Jela ya Kitui, kama jela zingine zote, lina tatizo la msongamano wa wafungwa. Jela ya Kitui yenye uwezo wa kubeba wafungwa 300, ilikuwa na wafungwa 673 jana asubuhi. Wengi wa wafungwa hao wameshtakiwa makosa madogo madogo ambayo faini yake labda haizidi Kshs5,000 ama Kshs10,000. Mwisho, wanabaki kukaa ndani wakipewa chakula na hawafanyi kazi yoyote."
}