GET /api/v0.1/hansard/entries/953984/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 953984,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/953984/?format=api",
    "text_counter": 94,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Faki",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13211,
        "legal_name": "Mohamed Faki Mwinyihaji",
        "slug": "mohamed-faki-mwinyihaji-2"
    },
    "content": "Jambo lingine ambalo tuliona ni kwamba pia mahakimu wana utepetevu mkubwa katika kuendesha kesi zao. Utapata zaidi ya kesi 100 katika gereza hili hazina tarehe za kusikizwa. Ikiwa huna tarehe ya kusikizwa, ina maana kwamba unakaa ndani lakini hujui ni lini utatoka. Iwapo umefungwa, unajua unatumikia kifungo cha miaka miwili kisha uende nyumbani. Kama unangojea kesi, hujui utatoka lini."
}