GET /api/v0.1/hansard/entries/954223/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 954223,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/954223/?format=api",
    "text_counter": 333,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Faki",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13211,
        "legal_name": "Mohamed Faki Mwinyihaji",
        "slug": "mohamed-faki-mwinyihaji-2"
    },
    "content": "Bw. Spika wa Muda, Mswada huu utakapopitishwa kuwa sheria, utasaidia pakubwa kuangazia uchumi wa utalii katika maeneo ya kaunti za Pwani. Ningependa kutoa masikitiko yangu kwamba Serikali Kuu haiweka mikakati yeyote ikishirikiana na serikali za kaunti kujaribu kufufua uchumi. Kwa mfano, ingekuwa bora kwa Serikali Kuu kupitia kwa Wizara ya Utalii, kuanzisha kongamano la kitaifa na kaunti zote 47 kuhusu mikakati ambayo wanapanga katika mambo ya utalii. Ilivyo kwa sasa, yale yanayofanywa na Serikali Kuu mashinani hayajulikani. Kwa hivyo, hakuna mwelekeo kamili unaotoka kwa Serikali Kuu kuhusiana na maswala ya utalii. Jambo la pili ambalo limeleta upungufu wa utalii ni kwamba hatujakuwa na bidhaa mpya za kitalii. Tumezoea bidhaa zile za kila siku, kama vile wanyama wa pori na fuo za bahari. Ndizo tunazotumia zaidi kujenga utalii wetu. Lakini, kuna sehemu zingine ambazo zina fuo nzuri za bahari, wanyama wazuri na barabara ambazo zinamfanya mtalii kutoka uwanja wa ndege mpaka makao anayokwenda ya maeneo ya utalii kwa urahisi zaidi kuliko ambavyo tunafanya hapa Kenya. Kwa mfano, ukishuka Mombasa na unataka kwenda Tsavo National Park inachukua masaa kuweza kufika na kuona wanyama. Kwa hivyo, ni muhimu turekebishe miundo msingi katika maeneo ya utalii."
}