GET /api/v0.1/hansard/entries/954231/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 954231,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/954231/?format=api",
"text_counter": 341,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Faki",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13211,
"legal_name": "Mohamed Faki Mwinyihaji",
"slug": "mohamed-faki-mwinyihaji-2"
},
"content": "Bw. Spika wa Muda, utalii katika maeneo ya Mombasa unaweza kuchangia pakubwa katika kujenga uchumi. Lakini, kama nilivyotangulia kusema, hakuna uwekezajia katika swala hili. Kwa mfano, ukienda katika hoteli ya English Point Marina, iko karibu sana na ufuo wa O ld Port ambao unahesabika kama mita 200 kutoka upande moja hadi mwingine. Lakini, hakuna mashua za kuchukua watalii kutoka sehemu moja hadi upande wa mjini ili watembee katika mji wa zamani wa O ld Port na baadaye wapande mashua na kuelekea upande wa pili na kurahisisha maswala ya usafiri. Pia, ukipanda ferry inachukua zaidi ya saa moja kutoka Nyali hadi mjini. Kwa hivyo, kama kutajengwa jeti ya kisasa na vijana wapewe mashua za kuendesha biashara, itasaidia pakubwa kupunguza umaskini na itakuwa rahisi kwa watalii kutoka kwa hoteli na kwenda katika maeneo ya kutazama. Katika mji wa Old Town, kuna Fort Jesus ambapo pana historia kubwa katika Mji wa Mombasa. Bw. Spika wa Muda, katika sehemu zingine kama vile Pwani ya kusini, mambo mengi ambayo yanaweza kufanywa na vijana ili kukuza utalii yanashindwa kufanyika kwa sababu ya ukosefu wa miundo msingi. Kwa hayo machache, naunga mkono Mswada huu. Ninaomba tumsaidie Sen. (Dkt.) Zani ili Mswada kupita."
}