GET /api/v0.1/hansard/entries/955471/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 955471,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/955471/?format=api",
    "text_counter": 320,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Faki",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13211,
        "legal_name": "Mohamed Faki Mwinyihaji",
        "slug": "mohamed-faki-mwinyihaji-2"
    },
    "content": "Asante, Bw. Naibu Spika, kwa kunipa fursa hii kuchangia Hoja ya kuundwa kwa kamati maalum ili kuchunguza mambo yanayohusu vifaa vya afya vinavyopelekwa katika kaunti. Kwanza, wazo la kuunda kamati ni nzuri sana kwa sababu kwa muda wa zaidi ya mwaka sasa, Bunge limekuwa likilalamika kuhusu mradi wa vifaa vya hospitali lakini hatujapata jibu lolote."
}