GET /api/v0.1/hansard/entries/955477/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 955477,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/955477/?format=api",
    "text_counter": 326,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Faki",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13211,
        "legal_name": "Mohamed Faki Mwinyihaji",
        "slug": "mohamed-faki-mwinyihaji-2"
    },
    "content": "Asante, Bw. Naibu Spika. Ijapokuwa wazo lenyewe ni nzuri, utekelezaji wake umekumbwa na utata kwa sababu Kamati ya Afya imekuwa ikizembea katika utendajikazi wake. Bw. Naibu Spika, wale watu waliochaguliwa kuwa wanakamati wa kamati hii maalum wengi wao wanatoka katika Kamati ambayo iko. Mwaka jana, tulipokutana na Waziri tarehe ishirini na saba mwezi wa kumi moja mwaka wa elfu mbili kumi na nane, maswala haya yalikuwa yako wazi na walikuwa na jukumu wakati ule wa kupambana nayo na kuhakikisha kwamba swala hili halirudi katika Bunge. Sijui ni matatizo gani ambayo yamekumba Kamati hii ya afya kuwa kakamavu katika kulifuatilia swala hili. Kwa hivyo, swala hili la vifaa vya afya ni swala ambalo lazima lifanyiwe utatuzi mapema kwa sababu kila mwaka mabilioni ya pesa zinatumiwa kulipia vifaa hivi wakati vifaa hivi vingi havifanyi kazi. Tumeona juzi katika hospitali kule Kwale vifaa ambavyo vimetolewa na vingine vimeharibika lakini hakuna juhudi zozote za kuvirekebisha na kaunti haziwezi kufanya marekebisho kwa sababu kuna mikataba ya kurekebisha vifaa vile wakati vinaharibika. Vifaa vingine vimewekwa kwa hospitali ambazo hazina maji safi lakini wameletewa mashini ya kusafisha damu yani dialysis machine. Kwa hivyo, mradi huu ni sawa na mradi Goldenberg lakini tutaita medicalberg kwa sababu inahusisha vifaa vya afya. Asante, Bw. Naibu Spika."
}