GET /api/v0.1/hansard/entries/955555/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 955555,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/955555/?format=api",
"text_counter": 404,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Madzayo",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 679,
"legal_name": "Stewart Mwachiru Shadrack Madzayo",
"slug": "stewart-mwachiru-shadrack-madzayo"
},
"content": "Bw. Naibu Spika, Katiba yetu inatuambia kwamba tutakapokuwa tunachaguguana, lazima tuangalie kila sehemu ya nchi hii, ili kuona kwamba watu wote wanapewa nafasi ya kufanya kazi kama hiyo. Lakini tukiangalia majina haya, hata kama Sen. Wetangula amesema kwamba walienda pamoja na Professor na wakaweza kuwashawishi wale wakubali, ingawa wengine walikataa na wengine walikubali. Lakini ikiwa swala kama hili linafanya jina lako linaanza kuharibika saa hii, na uko hapa ndani, basi afadhali ujiondoe. La mwisho, Bw. Naibu Spika, ikiwa wanachama wa Kamati hii hawataki kujiondoa, basi nafikiria nafasi iliyoko sasa ni kuchukua hatua ya sisi wenyewe kuwaondoa."
}