GET /api/v0.1/hansard/entries/956135/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 956135,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/956135/?format=api",
    "text_counter": 384,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Lamu East, JP",
    "speaker_title": "Hon. Ali Sharif",
    "speaker": {
        "id": 2100,
        "legal_name": "Shariff Athman Ali",
        "slug": "shariff-athman-ali"
    },
    "content": "Mzazi anapojifungua mtoto ina maana ya kwamba mtoto yule ameanza maisha yake. Malengo ni kwamba mtoto yule atalewa na mwishowe atahitaji kazi. Tunajua vizuri namna nchi yetu ilivyo. Mheshimiwa aliyeuleta Mswada huu ametambua kwamba kuna dharura ya kuwapatia akina mama wanaofanya kazi muda wa kutosha wanapojifungua ili wajipange namna watakavyowaelekeza watoto hao. Naamini kwamba muda ambao wamepewa ni wa takribani miezi mitatu. Ningependa vilevile akina mama hao, baada ya kupewa miezi hiyo mitatu, kuwe na namna ambayo watakuwa wanasaidika kikamilifu katika kuliangazia suala hili la watoto. Hii ni kwa sababu, utotoni mwa kila mtu ni wakati muhimu sana katika malezi."
}