GET /api/v0.1/hansard/entries/956136/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 956136,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/956136/?format=api",
    "text_counter": 385,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Lamu East, JP",
    "speaker_title": "Hon. Ali Sharif",
    "speaker": {
        "id": 2100,
        "legal_name": "Shariff Athman Ali",
        "slug": "shariff-athman-ali"
    },
    "content": "Hivi sasa, vijana wengi wako katika hali ya sintofahamu; hawajitambui ama kujielewa. Vijana hao pengine wametupwa na mama zao ama hawajui wazazi wao. Siku hizi idadi ya vijana ambao hawana kazi imekuwa kubwa zaidi kwa sababu ya tatizo hili ambalo lilianza hapo awali, na kwa sababu ya makosa ambayo hufanyika wakati mtoto anapozaliwa. Kwa hivyo, kuna dharura katika nchi hii ya kuwepo kwa mwongozo kamili wa kujua idadi kamili ya vijana wanaozaliwa, wanaoinuka, wanaosoma na hata wale ambao hawana kazi. Sielewi ni kwa sababu gani nchi hii haina watu wengi. Tukiangazia idadi ya wanaoishi katika nchi hii, ambao wamefikia kiwango cha kuwa na kazi zao ni takribani milioni 40 hivi lakini idadi ya wale ambao hawana kazi ni wengi sana. Hali hii pengine imesababishwa na kutokuweko kwa takwimu kamili ya kuonyesha ni vijana wapi…"
}