GET /api/v0.1/hansard/entries/956139/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 956139,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/956139/?format=api",
    "text_counter": 388,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Lamu East, JP",
    "speaker_title": "Hon. Ali Sharif",
    "speaker": {
        "id": 2100,
        "legal_name": "Shariff Athman Ali",
        "slug": "shariff-athman-ali"
    },
    "content": "Itakuwa vyema wakati kila jambo linaanza liwe na utaratibu. Linapoanza na makosa basi hata huko mbele mambo mengi yataenda mrama. Ni dharura kubwa kwa nchi hii kuangazia mwelekeo na mwongozo wa wananchi wake hususan vijana hapa nchini kwa sababu namna inavyoenda ni kwamba wengi wamekosa imani kabisa na nchi yao. Unapata wengine wanafanya mambo ambayo hayastahili, wengine wanajiingiza katika mambo mabaya na tabia ambazo si njema katika jamii. Kwa hivyo, kuna dharura kubwa hapa nchini ya kuweza kuangazia na kuwa na mipangilio kamilifu katika suala hili kwa wananchi na jamii."
}