GET /api/v0.1/hansard/entries/957048/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 957048,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/957048/?format=api",
"text_counter": 483,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Boy",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13200,
"legal_name": "Issa Juma Boy",
"slug": "issa-juma-boy"
},
"content": "Asante sana, mhe. Naibu Spika, kwa kunipa fursa hii ili niweze kuchangia na pia kuunga mkono huu Mswada wa County Revenue Bill. Kusema ukweli, siku zilizopita, kaunti zetu 47 zilikuwa zimesimama zote. Hakuna huduma yeyote inayofanyika, wafanyikazi wanalia na hakuna jambo lolote katika kaunti linaendelea isipokuwa ni kungojea pesa hizi zitoke. Kenya nzima inatutazama katika runinga siku ya leo. Sisi kama maseneta katika hizi kaunti 47, Kwale ikiwa mojawapo, mimi naunga mkono Mswada huu lakini pesa hizi si za kuwafaidisha magavana."
}