GET /api/v0.1/hansard/entries/957107/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 957107,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/957107/?format=api",
    "text_counter": 542,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Faki",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13211,
        "legal_name": "Mohamed Faki Mwinyihaji",
        "slug": "mohamed-faki-mwinyihaji-2"
    },
    "content": "Asante Bw. Naibu Spika kwa kunipa fursa kuchangia Mswada wa ugavi wa rasilimali kwa kaunti zetu. Kwanza ningependa kupongeza Kaunti ya Kitui na Seneta wao, Sen. Sen. Wambua, kwa makaribisho mazuri ambayo tumepewa. Jambo la pili ni kwamba sisi katika Kenya tuna Katiba lakini hatuna ukatiba. Hatuna ukatiba kwa sababu hatuheshimu sheria na utengamano katika nchi yetu. Ndio unaona kwamba katika kila sehemu kuna matatizo kadha wa kadha. Tunalalamika lakini Bunge bado linafanya yale amabayo linafanya. Tunalalamika kuwa bado Magavana wanawaibia wananchi pesa zao. Vile vile tunalalamika kwamba hatuna usawa katika ugawaji wa rasilimali za nchi hii. Nikikupa mfano wa Mombasa, mwaka jana tulipewa Kshs8.2 billioni. Mwaka huu tunapewa Kshs7,025 billioni, upungufu wa zaidi ya Kshs1.2 billioni. Hiyo inamaana kwamba ile mipango iliofanyika mwaka jana haitaweza kufanyika katika mwaka unaofuata. Pia ina maana kwamba maendeleo yatarudi nyuma katika Kaunti ya Mombasa. Sasa hivi, uchumi wa Mombasa umeathiriwa pakubwa na reli ya Standard Gauge"
}