GET /api/v0.1/hansard/entries/957109/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 957109,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/957109/?format=api",
"text_counter": 544,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Faki",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13211,
"legal_name": "Mohamed Faki Mwinyihaji",
"slug": "mohamed-faki-mwinyihaji-2"
},
"content": "Railway (SGR) ambapo Serikali imetoa maagizo kwamba mizigo yote ibebwe na reli kutoka Mombasa mpaka Nairobi na baadaye hadi Naivasha. Katika Kaunti ambazo zinazalisha rasilimali zaidi katika nchi ya Kenya ni Nairobi, Kiambu, Nakuru na Mombasa. Tukiangalia zingine zote tatu zimeweza kupata ongezeko katika rasilimali ambazo zinapelekwa na Serikali Kuu katika kaunti hizo. Hatujui ni dhambi gani Mombasa ilifanya isiweze kupata rasilimali kama wanavyopata wengine. Nikiangazia swala la revenue, juzi tulipokua Mombasa tulielezwa na Kaunti kwamba wameweza kupata revenue kupita kiasi ambacho walipata mwaka uliokwisha. Kwa hivyo maswala ya revenue sio kigezo peke yake cha kuhakikisha kwamba pesa zinakwenda sawa sawa. Kama hali hii haitaweza kudhibitiwa, miaka mitano ijayo, mji wa Mombasa utakua umekufa na Kaunti hio itakua imekufa. Mombasa ikifa, kaunti za Kilifi, Lamu, Kwale, Taita-Taveta na Tana River zote zitaathirika. Hospitali kuu ambayo inatumika Pwani nzima iko katika Kaunti ya Mombasa. Kwa hivyo, kama tunafuata Katiba lazima ugavi wa rasilimali uwe sawa. Kama Mombasa huikuweza kupata zile pesa ambazo walipaswa kukusanya, wangepewa zile ambazo walipewa mwaka jana, si wapunguziwe kwa kiwango cha Kshs1 billion katika ugavi wa mwaka huu. Bw. Naibu Spika kumekuwa na manungāuniko kwamba Seneti haichukui hatua dhidi kwa Magavana wanaofanya uharibifu wa---"
}