GET /api/v0.1/hansard/entries/957115/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 957115,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/957115/?format=api",
"text_counter": 550,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Faki",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13211,
"legal_name": "Mohamed Faki Mwinyihaji",
"slug": "mohamed-faki-mwinyihaji-2"
},
"content": "Bw. Naibu Spika, tumeambiwa kwamba Seneti haiumi katika maswala ya magavana wanaoiba rasilimali. Tulipoenda Samburu, siku ya pili Gavana alishikwa. Kwa hivyo, tunataka viungo vingine vya Serikali kama Ethics Anti-Corruption Commission (EACC) na Directorate of Criminal Investigations (DCI) viwe macho zaidi, kwa sababu wao ndio wana uwezo wa kuchunguza na kushika watu wanaohusika katika maswala kama haya. Hata Seneti ikimpata Gavana wa hapa akiwa na hatia, hatuna nguvu ya kumshika na kuhakikisha kwamba amepelekwa katika kituo cha polisi na ashitakiwe. Mwisho, mahakama lazima iwe imara. Juzi Uingereza kulikua na tatizo la Bunge kuhairishwa. Mmoja wa Wabunge alienda kortini; korti ya kwanza ikakataa na ya pili ikakubali kwamba Waziri Mkuu alikuwa amefanya makosa. Sisi tulipeleka kesi miezi miwili iliopita na bado korti haijaamua ni nani atakaye sikiza kesi hiyo, na tunapaswa kuheshimu mahakama. Tutaheshimu vipi mahakama wakati inafanya ulegevu kama huo? Asante, Bw. Naibu Spika."
}