GET /api/v0.1/hansard/entries/957179/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 957179,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/957179/?format=api",
"text_counter": 614,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Wario",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13224,
"legal_name": "Golich Juma Wario",
"slug": "golich-juma-wario"
},
"content": "Asante, Bw. Naibu Spika, kwa kunipa nafsi hii nami niweze kuongeza sauti yangu. Nami pia naunga mkono katika hali ya kujivuta, kwa Mswada huu ambao tunaka kupitisha. Sisi kama Seneti tuliandamana na tukatembea huko Nairobi tukienda kortini ili kupigania haki ya waliotuchagua. Katika ile hali ambayo sisi tulikuwa tunapigania - kama vile Sen. Pareno alivyosema- tulikwa tunafanya kichapo cha mbwa kuingia msikitini, kupitia hali ya kisheria na sio hali ya nguvu wala mabavu. Bw. Naibu Spika, rasilmali ambazo tunapeleka katika maeneo yetu zinaendelea kudorora kwa sabbau, kutoka mwaka jana, pesa zinazidi kuwa kidogo tunavyosonga. Ukitaka kupima ili ujue kuwa kitu fulani kinaelekea kufifia, utaona ya kwamba, rasilmali hiyo, haiongezeki, ila inazidi kupungua. Rasilmali hii tunapelekea wananchi waliotuchagua na ambao wanazihitaji zaidi huko mashinani kwenye kaunti, Hatupeleki rasilmali kwa wahuni na magavana ili waende kuitumia vibaya. Hii ni mali ya watu maskini ambao wametuchagua walioko kule mashinani. Mengi yamezungumziwa, lakini ningependa kuwapongeza watu wa Kaunti ya Kitui pamoja na Seneta wao ambaye ni rafiki yangu. Ukitembea kidogo tu kutoka hapa, utafika Kaunti ya Tana River. Sisi ni majirani na ingekuwa vizuri tunapotoka hapa tuende"
}