GET /api/v0.1/hansard/entries/957214/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 957214,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/957214/?format=api",
    "text_counter": 649,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Mwaruma",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13223,
        "legal_name": "Johnes Mwashushe Mwaruma",
        "slug": "johnes-mwashushe-mwaruma"
    },
    "content": "Asante, Bw. Naibu Spika, kwa kunipa fursa hii ili nichangie Mswada huu ama sheria hii ya kugawa pesa kwa serikali za kaunti. Kwanza, ningependa kutumia fursa hii kukemea ile mbinu ambayo ilikuwa inatumiwa na Serikali ya Kitaifa kupimia hewa ugatuzi kwa kupunguza ule mgao wa pesa zinazoenda kwa ugatuzi. Wenye Serikali kuu walisema kwamba ndio wenye pesa na wataamua ni pesa ngapi zitaenda kwa serikali za kaunti. Kwa kweli wahenga hawakukosea waliposema ya kwamba, aliye nacho ni adui wa asiye nacho. Pia, ningependa kushukuru Serikali ya Kaunti ya Taita Taveta kwa sababu ya bidii waliyotia ya kukusanya pesa ama ushuru kutoka kwa gatuzi, kwa kizungu hali maarufu, Own-source revenue na kufanya gatuzi la Taita Taveta kupata mgao mwaka huu ukazidi Kshs400 milioni. Jukumu letu sasa ni kufaya bidii na kujifunga kibwebwe, kuangalia kwamba huu ugatuzi haujapimiwa hewa na haujaisha vile ilivyo kuwa katika serikali za majimbo za miaka ya 1966. Bw. Naibu Spika, sisi tuliotoka katika makabila madogo madogo, tulipigana kwa sababu tuliachwa nyuma kimaendeleo tulipokuwa tunaulizwa kwamba: ―Ninyi ni wachache sana, mnaleta kura ngapi katika meza?‖ Kwa hivyo, tukafinywa kwa upande wa kuletewa maendeleo. Nikiwa Seneta wa Taita Taveta, ninaunga mkono ugatuzi. Mbinu yeyote ambayo ni ya kuua ama kupimia pumzi ugatuzi ni kitu ambacho kinatakikana kukemewa sana. La pili, namuunga mkono Seneta wa Homa Bay, Mhe. M. Kajwang‘, aliposema ya kwamba kuna umuhimu wa kufanya costing ama kuangalia ile sheria ya PublicFinance Management (PFM)Act kando ya ile sheria ya County Allocation of RevenueAct (CARA) katika kuweka ceilings za pesa zinazoenda kwa assemblies . Kwa hakika, kuna assemblies zingine ambazo zinapata pesa wasizohitaji. Na pale ndipo kuna kupoteza pesa nyingi sana zinazoenda kwa ugatuzi. Inatakikana kufanywe valuation ama"
}