GET /api/v0.1/hansard/entries/958391/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 958391,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/958391/?format=api",
    "text_counter": 52,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Kinyua",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13202,
        "legal_name": "John Kinyua Nderitu",
        "slug": "john-kinyua-nderitu-2"
    },
    "content": "Asante sana Bw. Spika, kwa kunipa fursa hii. Ninasimama kusema ya kwamba, maneno yaliyosemwa na Seneta wa Kaunti ya Kitui ni ukweli mtupu. Kamati ambayo inahusika na usalama inapaswa izingatie, sio hio sehemu pekee yake, lakini pia Laikipia. Hawa wezi wa mifugo wamekuwa kidonda sugu. Ukienda sehemu za Kinamba,Wangwashe na El Moran, imekuwa kila wakati watu hawalali na kazi yao imekuwa kufuata wezi wa mifugo. Jambo ambalo linavunja moyo ni kwamba, Waziri wa Usalama aliwapokonya vijana ambao walipewa bunduki kihalali na Serikali kwa kisingizio ya kwamba, wanaenda kuangalia jinsi hizo silaha zilipeanwa. Tungependa Kamati inayohusika na usalama ifuatilie kwa mapana na marefu ndiyo tuweze kujua kisa na maana ya huu usalama. Tumekuwa tukizungumzia mambo ya usalama katika nchi hii yetu ya Kenya kila wakati, usiku na mchana na tunaona kana kwamba, hakuna jambo lolote linalotendeka. Asante sana, Bw. Spika."
}