GET /api/v0.1/hansard/entries/958394/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 958394,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/958394/?format=api",
"text_counter": 55,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Faki",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13211,
"legal_name": "Mohamed Faki Mwinyihaji",
"slug": "mohamed-faki-mwinyihaji-2"
},
"content": "Asante Bw. Spika, kwa kunipa fursa hii kuchangia Arifa iliyotelewa na Seneta wa Kitui; Sen. Wambua. Usalama wa nchi na mali yao ni jambo muhimu sana kwa taifa. Ni jukumu la kwanza kabisa la serikali yoyote kuhakikisha kwamba kuna usalama wa mali na wananchi katika nchi yake. Visa vya mauaji kama hayo yaliyotokea Kitui, yametokea Taita na sehemu zingine za nchi. Ni muhimu tuone kwamba yale mapendekezo ya community policing yanatekelezwa. Hii ni kwa sababu mauaji haya mengi yanatokea katika maeneo ambayo wananchi wanaishi katika kaunti zetu. Iwapo hatutachukua hatua za haraka, kila sehemu itapata matatizo ya ukosefu wa usalama. Haiwezakani kwamba raia alalamike kuhusiana na mifugo kuingia katika shamba lake, na adungwe mkuki na afariki. Ni jambo ambalo lazima tutilie maanani na lichukuliwe kama jambo la uzito. Mtu anapopoteza maisha sio jambo ndogo kwa sababu anaacha familia na watoto wanapata shida. Kwa hivyo, hili ni jambo ambalo kamati husika lazima iangalie. Vita dhidi ya ukosefu wa lisho kwa mifugo na mifugo kurandaranda ni jambo ambalo linaathiri kaunti zote katika nchi ya Kenya. Asante, Bw. Spika."
}