GET /api/v0.1/hansard/entries/958458/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 958458,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/958458/?format=api",
"text_counter": 119,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Faki",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13211,
"legal_name": "Mohamed Faki Mwinyihaji",
"slug": "mohamed-faki-mwinyihaji-2"
},
"content": "Asante, Bi. Spika wa Muda, kwa kunipa fursa hii kuunga mkono Arifa ya Sen. (Dr.) Musuruve. Ningependa kumpongeza Sen. (Dr.) Musuruve kwa kutetea haki za wale ambao hawakubahatika katika jamii, hususan wale ambao ni walemavu. Wengi wetu hatukuwa tunajua kuwa kuna mwezi maalum ambao unahadhimisha siku ya viziwi. Lakini kwa uwezo wake ametuelimisha na sisi pia tutaendelea kuwaelimisha wengine ambao walikuwa hawajui swala kama hili. Tukiangalia hata sisi katika Bunge la Seneti na Bunge la Kitaifa, hakuna mkalimani wa lugha ya ishara ambaye anatafsiri mazungumzo ambayo yanaendelea katika Bunge kwa wale ambao hawasikii katika jamii. Kwa hivyo, kama Bunge la Seneti, tumeacha nyuma sehemu kubwa ya jamii yetu ambao wangeweza kufurahia na kusikiza yale ambayo yanaendelea katika Bunge kama hili na Bunge la Kitaifa. Nafikiri kwa kuadhimisha swala hili, tunapoenda Kitui wiki ijayo, ni lazima kwa mwezi huu tupate mtaalamu mmoja wa lugha ya ishara ili aweze kutafsiri majadiliano ambayo yanaendelea katika Bunge letu. Asante, Bi. Spika wa Muda."
}