GET /api/v0.1/hansard/entries/959577/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 959577,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/959577/?format=api",
    "text_counter": 347,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Faki",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13211,
        "legal_name": "Mohamed Faki Mwinyihaji",
        "slug": "mohamed-faki-mwinyihaji-2"
    },
    "content": "Asante Bi. Spika wa Muda, kwa kunipa fursa ya kuchangia azimio la upanzi wa miti ambalo limeletwa Seneti na Sen. Kibiru, Seneta wa gatuzi la Kirinyanga. Ninampongeza Sen. Kibiru kwa fikira zake na kuleta azimio kama hili. Kwa sasa, kuna umuhimu mkubwa wa kupanda miti, kuboresha na kurudisha mazingira kwa sababu ya changamoto la ongezeko la joto ulimwenguni, kwa jina lingine global warming . Juzi kulitokea kibunga katika nchi ya Bahamas iliyoko kusini mwa Amerika. Sababu kubwa ilisemakana kwamba ni tatizo la ongezeko la joto ulimwenguni. Kwa hivyo, upanzi wa miti utasaidia pakubwa kupambana na tatizo la ongezeko la joto ulimwenguni na vilevile kurudisha na kuboresha mazingira ambayo tunaishi nayo katika wakati wa sasa. Bi. Spika wa Muda, kwa muda mrefu sasa, miti mingi ya kiasili imekatwa kiholela ili watu wapate sehemu za ukulima, makao na mbao ambazo zinatumika kutengeneza vitu tofauti tofauti. Lakini, hakujakuwa na mradi ambao unatarajiwa kurejesha mazingira kama ilivyokuwa zamani. Wakati Rais mstaafu Daniel arap Moi alikuwa uongozini kulikuwa na siku maalum kila mwaka ya kuadhimisha upanzi wa miti katika nchi yetu ya Kenya. Lakini, kwa sasa, kutoka atoke mamlakani, hakujakuwa na harakati zozote za kuhakikisha kwamba miti inapandwa katika Jamhuri yetu ya Kenya. Vile vile, juzi katika vyombo vya habari kulikuwa na mjadala mkubwa kuhusiana na uchomaji wa misitu katika eneo la Amazon kule Brazil, Amerika Kusini. Bi. Spika wa Muda, kuna juhudi kubwa sasa ambayo inafanywa na nchi za kimataifa ili kuhakikisha kwamba mazingira katika Msitu wa Amazon yanarejeshwa ili kuhakikisha kuwa miti inaendelea kukua na kusaidia pakubwa kupunguza joto ulimwenguni."
}