GET /api/v0.1/hansard/entries/959586/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 959586,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/959586/?format=api",
"text_counter": 356,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Faki",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13211,
"legal_name": "Mohamed Faki Mwinyihaji",
"slug": "mohamed-faki-mwinyihaji-2"
},
"content": "Bi. Spika wa Muda, kwa kumalizia ningependa kuchangia swala la DORA. Waswahili wanasema heri nusu shari kuliko shari kamili. Nusu ya shari ni kwamba tumeweza kukubaliana kwamba Kaunti zipewe Kshs316.5 billion . Shari kamili ni kwamba tulikuwa katika mazingira ambayo wafanyikazi wengi wa Kaunti nchini kote walikuwa hawapati mishahara kwa wakati unaofaa. Kwa hivyo, kama Seneti tumeweza kukubali na kuzingatia kwamba wananchi wengi wanapata shida. Wengine wameshindwa kurejesha wanafunzi katika muhula wa tatu wa shule ambao umeanza wiki iliyopita. Vile vile, wengine wameshindwa kupata ruzuku kwa sababu ya ukosefu wa mishahara kwa wakati ufaao."
}