GET /api/v0.1/hansard/entries/959774/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 959774,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/959774/?format=api",
"text_counter": 178,
"type": "speech",
"speaker_name": "Baringo CWR, KANU",
"speaker_title": "Hon. (Ms.) Gladwell Cheruiyot",
"speaker": {
"id": 13231,
"legal_name": "Gladwell Jesire Cheruiyot",
"slug": "gladwell-jesire-cheruiyot"
},
"content": " Asante sana, Mhe. Naibu Spika wa Muda kwa kunipatia nafasi ili pia nichangie Mswada huu ambao umeletwa na Mhe. Jude Njomo. Hata kama jina si langu, kuna Mheshimiwa mmoja alikuwa amesema anaitwa Judy Njomo. Nadhani yeye si Judy lakini ni Mhe. Jude Njomo. Mimi pia naungana na wale ambao wanasema Mswada huu ni muhimu. Sisi Wakenya tumepitia mambo mengi kupitia kwa fedha ambazo tunaomba katika benki zetu. Watu wetu waliumia sana tulipokuwa tumepatia benki zetu nafasi kubwa ziweze kufanya kazi jinsi ambavyo zinafikiria. Ni jambo zuri kuona kwamba Bunge hili la 12 limepewa nafasi na Mahakama Kuu ya Kenya wakati ambapo mtu mmoja anayeitwa Boniface Oduor alipoenda kortini kusema kwamba Mswada uliopitishwa na Bunge la 11 kwamba watu wanapoomba pesa, wapewe kiwango fulani ambacho wanaweza kumudu… Bw. Oduor alishirikiana na wengine kwenda kortini ili waweze kusimamisha jambo hilo na wazipatie nafasi benki zetu zitoze watu ushuru ule wanataka wao wenyewe. Limekuwa jambo la kusikitisha mimi nikiwa mama wa Kaunti ya Baringo ninapopata simu za kina mama wakinipigia wakilia jinsi ambavyo wanatozwa pesa wakiwa wanauza mboga. Wako na shida nyingi maana wanaitishwa fedha ambazo hawana. Zile kidogo wako nazo wananyang‟anywa. Hata ng‟ombe wao wanachukuliwa na wanakuwa na maisha hohe hahe kwa sababu ya hii mikopo ambayo wanaomba kwa shylocks, ambayo hawajapatiwa njia ya kufanya kazi inavyoweza kufaidi Mkenya wa kawaida. Ni vizuri kujua kwamba Bunge hili limepewa miezi 12 ili kuangalia Mswada huu na tuubadilishe ili uweze kumfaa Mkenya wa kawaida. Ni vizuri tumshukuru Mhe. Jude Njomo maana amekuja mbele hapa ili tuweze sote kusaidiana kuona kwamba Mswada huu umepita. Ni kweli kwamba wajenzi na wafanyabiashara wakubwa nchini humu wameumia sana maana hawawezi kuomba fedha za kufanya biashara na biashara nyingi zimeenda kule China. Fedha nyingi zinatoka nje ya Kenya ndiposa hapa Kenya tunalia kwamba hakuna pesa. Kama fedha hizo zinatoka nchi hii na kupelekwa nchi zingine, itakuwa si vyema kwa sababu watoto wetu ambao hawana kazi wangenufaika iwapo fedha hizo zingebaki hapa. Pesa hizo pia zingetusaidia kufanya biashara kubwa kubwa hapa nchini kama kujenga na kufanya mambo mengine. Inasikitisha unaposikia kwamba huko Uchina wanatozwa riba ya asilimia 4. Huku kwetu, tunaitisha asilimia 18 hadi 20. Hakutakuwa na ushindani kwa hali inayofaa. Inafaa tuangalie ili The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposes only. Acertified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}