GET /api/v0.1/hansard/entries/959775/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 959775,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/959775/?format=api",
    "text_counter": 179,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Baringo CWR, KANU",
    "speaker_title": "Hon. (Ms.) Gladwell Cheruiyot",
    "speaker": {
        "id": 13231,
        "legal_name": "Gladwell Jesire Cheruiyot",
        "slug": "gladwell-jesire-cheruiyot"
    },
    "content": "tuweze kuwafaidisha Wakenya kwa sababu Kenya ni nchi ambayo bado inaendelea. Hatujafika kiwango ambacho tunasema kwamba tumeweza kujimudu. Ni vizuri kuangalia miswada ambayo inafaidi mkenya ili Kenya iweze kunawiri. Mimi nimependa Mswada huu kwa sababu kuna mahali unasema kwamba yule mtu anayesimamia benki ndiye anayeweza kuulizwa ajitokeze aseme sababu zilizomfanya aende kinyume na sheria ambayo itawekwa ya benki. Hii ni muhimu kwa sababu hapo mbeleni ilikuwa inasemekana tu benki na haikuwa inawekwa kwa yule mtu anayesimamia benki hiyo, iwapo wataenda kinyume cha sheria na kazi ambayo imetengwa na Bunge hili ama sheria zetu. Nimesikia Mhe. Jude akisema kwamba kuna shida katika nchi hii kwa sababu wale watu ambao wanarithi pesa ambao kwa Kiingereza wanaitwa next of kin katika ule uwekezaji wa fedha, Mpesa na hata hii inaitwa Tala na Fuliza, hakuna mtu anayejua kabisa kinachoweza kutendeka. Iwapo mimi kama Mhe. Gladwell kwa bahati mbaya, na Mungu anirehemu nisipate shida, nipate kwamba sina maisha tena, tuko na uhakika gani kwamba benki itawaita watu ambao nimewaandika kama next of kin waambiwe: “Mhe. Gladwell alikuwa na pesa kiwango fulani kwa benki yetu na kwa hivyo yule ambaye ameachiwa fedha hizi ni wewe?” Tunataka Auditor-General, kama hii kazi iko mbele yake, pia atueleze katika hii miaka ambayo tuko, benki zetu zimebaki na pesa kiwango gani ambazo zinadaiwa na wale watu wanaitwa next of kin . Hapo pia pana shida. Watu wanakufa na kuwacha simu zao zikiwa na fedha. Hizo pesa zinaenda wapi? Hayo ni baadhi ya mambo ambayo tunataka kusikia yameangaliwa ili Wakenya wasikae wakiwa na hofu. Ndiyo sababu unaona watu wengine wanaweka pesa zao kwenye godoro. Mswada huu umekuja kwa wakati unaofaa. Mambo ya uombaji wa pesa kupitia simu unaofanywa na watoto wetu ambao ni wanafunzi umewaathiri wazazi wengi, mimi nikiwa mmoja wao. Kila wakati mtoto anakwambia “Mama niko na deni.” Mara wanasema: “Usiweke kwa hii laini, wacha ninunue laini nyingine” au “Tuma kwa rafiki yangu”. Sijui inafaidi nini nchi hii ikikopesha watu pesa ambazo kiwango chao cha riba ni cha kila mwezi na sio cha kila mwaka. Kiwango hicho cha riba kiko juu. Kinawaumiza sisi wazazi kwa maana watoto wanapoenda kuomba fedha, hawahitajiki kudhibitisha kwamba wanafanya kazi au la. Bora tu una nambari ya simu, unaweza kuomba pesa na hawajui mtoto atalipa vipi pesa ile. Inakuwa kwamba bado tu ni mzazi ambaye atalipa fedha ikiwa ni Tala, Fuliza au nyingine. Ni muhimu kwamba CBK iweze kusimama imara ili kuweza kulainisha mambo ambayo yanasumbua Mkenya. Haifaidi kitu iwapo benki ambayo labda iko na watu 1,000 inafaidika na uombaji wa pesa kupitia pesa wanazotoza Wakenya na Wakenya wanaumia kila uchao. Ni muhimu kusema kwamba wakati huu ambapo mwezi huu unakaribia kuisha, bado kuna Wakenya ambao hawajabadilisha fedha za zamani. Ni muhimu benki zetu ziwakumbushe watu au wawekezaji wao waweze kurudisha pesa hizo. Nilikuwa ninatazamia kuona runinga zetu zikieneza taarifa hii lakini hilo halijafanyika. Katika Bunge hii la 12, nimewasikia wenzangu hapa wakisema kwamba, kwa sababu Rais wa nchi hii pia anafanya biashara ya benki, wako na hofu kwamba anaweza kukataa kupitisha Mswada huu. Si vyema kuanza kufikiria kwamba kuna jambo kama hilo. Ni vizuri tuwe na tumaini kwamba Rais wetu ana moyo wa kusaidia Wakenya na iwapo tutapitisha Mswada wetu, atauangalia kwa kindani na kuupitisha ili tuwasaidie Wakenya."
}