GET /api/v0.1/hansard/entries/960100/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 960100,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/960100/?format=api",
"text_counter": 265,
"type": "speech",
"speaker_name": "Lamu CWR, JP",
"speaker_title": "Hon. (Ms.) Ruweida Obo",
"speaker": {
"id": 786,
"legal_name": "Ruweida Mohamed Obo",
"slug": "ruweida-mohamed-obo"
},
"content": " Asante, Mhe. Naibu Spika wa Muda. Naunga mkono moja kwa moja maana usalama wetu ndani ya ndege ni muhimu sana. Sheria ziko nyingi. Hii leo kampuni nyingi zinazingatia zaidi mambo ya usalama. Kuna laini ndefu. Usalama huanza pale wageni wakiingia ndani ya ndege, mizigo ikichukuliwa na hata tukiwa ndani ya ndege. Usalama unatakikana katika nyanja zote hata ndege inapopaa. Kutoka ndege ikipaa angani mpaka inaposhuka usalama unahitajika wakati wote. Mtu akianza kuleta shida ya usalama, captain au rubani wa ndege ana haki⦠Amepewa jukumu na sheria. Hata kama ni nani amebebwa humo ndani, yeye ndiye captain, yaani rubani. Anayo haki ya kuirejesha ndege haijalishi nani yuko ndani. Yeye ndiye mwamuzi wa mwisho. Mambo mengi kuhusu usalama yametokea sehemu nyingi na hata kuhatarisha maisha ya watu. Huwa ni kwa sababu ya mtu mkorofi ama mlevi. Ndege inapofanya emergency landing huwa ni hasara kubwa kwa sababu mafuta huwa yametumika mengi. Charges zimetozwa kwa kushuka kwa ndege. Kwa Kimombo zinaiitwa landing fees and air navigation fees . Zote hizo huwa zimetozwa. Ni hasara nyingi. Wale waliopo kwenye ndege wanataka utulivu na usalama. Nikisema usalama, nawaonya wale, pengine kwa kutojua au kujua, wanaleta hatari kwa sababu itakufikia wewe mwenyewe pia. Unafanya wengine kama wahudumu wa ndege na marubani wawe na kazi nyingi zaidi. Kuna zile"
}