GET /api/v0.1/hansard/entries/960103/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 960103,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/960103/?format=api",
    "text_counter": 268,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Lamu CWR, JP",
    "speaker_title": "Hon. (Ms.) Ruweida Obo",
    "speaker": {
        "id": 786,
        "legal_name": "Ruweida Mohamed Obo",
        "slug": "ruweida-mohamed-obo"
    },
    "content": "akatoka kwa kikapu, watu wakasongea upande mmoja na ndege ikaanguka. Wakati mwingine abiria anaweza kuleta fujo mpaka kupigana, watu wasonge upande mmoja, kukakosa ule usawa wa ndege na ndege huenda ikaanguka. Ni muhimu kuwa na usalama wa ndege, abiria na mizigo. Kuna mengi ya kusema lakini naunga mkono usalama uwepo. Lakini pia tusiangalie tu usalama ndani ya ndege. Usalama ni wingi kwa ndege. Kwa mfano, Serikali yetu ya Kenya au Wizara husika ya Uchukuzi inafaa iangalie vifaa vinavyotumika kwa ndege viwe vya kisasa. Kwa mfano, kuna kifaa ambacho kinaitwa VHF omnidirectional range (VOR). Hicho kinafaa kisaidie ndege katika kupaa kwake ama kushuka pale Mombasa. Lakini kifaa hicho kinatumika zaidi wakati wa mvua. Hivi vifaa vya Kenya, havifanyi kazi wakati wa mvua. Kifaa hicho kinatumika tu wakati wa jua. Pale unapokihitaji zaidi, huwezi kukitumia. Naomba waangalie vile vifaa vinavyohitajika katika viwanja vya ndege vyetu vyote kwa sababu vinachangia pakubwa katika usalama. Wahakikishe vinafanya kazi wakati vinahitajika. Sisi tulivipatia jina wakati tukiruka. Badala ya kuviita Mike Oscar Victor, tunaviita Mike Oscar Vision kwa sababu unavitumia wakati unaweza kutembea ukiona. Wakati huoni na unahitaji kifaa hicho ndio haukipati. Ningependa Serikali na wizara husika ziangalie viwanja vyetu vya ndege. Viwanja vyetu vya ndege vinasikitisha. Sehemu nyingine zina mipangilio kutoka nje mpaka ndani. Yote hayo yanachangia usalama. Maanake abiria akiwa na hasira pengine amefanyiwa vibaya pale nje, akiingia ndani ana hasira na kuelekeza hasira mpaka kwa ndege. Pale nje, madereva wa taxi wanakaa kama sokoni. Wanakuvuta huku na kule ukitoka ni kama hakuna tofauti na Soko la Kongowea, Mombasa. Ukitoka kila mtu anakuvuta huku, wengine wanakushika mkono kabisa wanakuvuta kule. Sisi Wakenya hatuko mbele. Ukienda katika nchi yoyote, picha ya kwanza unayopata ni kwa kiwanja cha ndege. Unapata picha ya watu walio na tabia hiyo. Wageni wakiingia tunaonekana hatujipangi vizuri. Nchi zingine za Afrika utaona ukiingia, taxi zinaingia kwa laini. Hakuna shida kutoka ukiingia kwa gate mpaka mwisho. Huku unaweza kukasirishwa huku na kule mpaka ukifika ndani umechoka, sasa nawe hasira zako umepeleka kwa ndege. Kuna mengi ya kuangaliwa katika ndege. Kama rubani, mimi ni mmoja wao. Kuna"
}