GET /api/v0.1/hansard/entries/960175/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 960175,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/960175/?format=api",
    "text_counter": 340,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Lamu CWR, JP",
    "speaker_title": "Hon. (Ms.) Ruweida Obo",
    "speaker": {
        "id": 786,
        "legal_name": "Ruweida Mohamed Obo",
        "slug": "ruweida-mohamed-obo"
    },
    "content": " Asante. Mhe. Naibu Spika wa Muda, tumechangia sana. Ningependa kuchukua nafasi hii pia kupongeza KCAA. Nimetoka hapo nje kupiga simu kwa marubani kadhaa kuwauliza kama pengine kuna shida zaidi kwa sababu mimi sijarusha ndege kwa miaka kama miwili. Wameniambia saa hii KCAA wanafanya kazi nzuri na kwamba wamefunga ukanda. Zaidi ni kwamba kutoka tupate ile safari ya kwenda Amerika, wamejaribu zaidi. Sehemu nyingi wameziba mashimo. Hiyo ni kazi nzuri. Nawapongeza sana KCAA. Tukizungumzia mambo ya ndege na viwanda, itakuwa si vyema watu wa Lamu wakiniangalia nikiyazungumzia hayo. Katika Kaunti ya Lamu, kiwanja cha ndege ni kimoja. Kitambo, ungeweza kutoka nchi za nje na uingie humu nchini kupitia Lamu. Saa hii, hauwezi kwa sababu ya mambo ya usalama. Tunaomba Kamati hii izingatie jambo hili. Wacha niseme kwa kimombo ili mwenyekiti aelewe. Wakati wa nyuma, Lamu ilikuwa entry and exit point . Saa hii, hatuna hilo na tumeendea mambo ya kaunti. Inafaa kaunti zote 47 ziwe na viwanja vya ndege vya kimataifa. Kuna visiwa upande wa Lamu Mashariki. Katika nchi nyingine, utapata kila kisiwa kina kiwanja cha ndege. Ni masikitiko kwamba Lamu tuna visiwa 11 na havina viwanja vya ndege. Wakati wa nyuma, visiwa vya Pate, Ndau and Kiwayu vyote vilikuwa na viwanja vya The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposes only. Acertified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}