GET /api/v0.1/hansard/entries/960176/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 960176,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/960176/?format=api",
    "text_counter": 341,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Lamu CWR, JP",
    "speaker_title": "Hon. (Ms.) Ruweida Obo",
    "speaker": {
        "id": 786,
        "legal_name": "Ruweida Mohamed Obo",
        "slug": "ruweida-mohamed-obo"
    },
    "content": "ndege. Saa hii vyote havina viwanja vya ndege. Saa hii, kukitokea mgonjwa usiku na bahari ni chafu au mgonjwa akitakikana kuletwa Nairobi kwa ndege… Sehemu kama vile Maasai Mara kunawekwa mataa ili ndege zishuke kumchukuwa mgonjwa ambaye anatakikana kusafirishwa hadi Nairobi. Lamu, hilo haliwezekani hata tukitaka. Ni mpaka mtu apitie bahari chafu na shida nyingi. Naomba Kamati hii izingatie mambo hayo. Haiwezekani kuwa na kisiwa ambacho kina watu zaidi ya 18,000 na kiwe hakina kiwanja kidogo cha ndege ambapo ndege ndogo ndogo zinaweza kutoa mtu wakati wa dharura. Hata kuhusu usalama, najua eneo la Lamu lilivyo. Itawasaidia sana watu wa Lamu kama kutakuwa na viwanja vya ndege hata huko mainland . Vitasaidia watu kusafiri na kufika kwa haraka. Kwa mfano, kama mtu amechukuliwa au imetokea dharura yoyote ya usalama, wataruka kwa haraka na wafike. Naomba sana hilo lifanyike. Naona mwenyekiti yuko hapa. Namuomba jambo hili alitilie mkazo. Kisiwa chochote… Hata kule Kisumu inafaa kuwe na airport moja. Asante, Mhe. Naibu Spika wa Muda."
}