GET /api/v0.1/hansard/entries/960430/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 960430,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/960430/?format=api",
"text_counter": 241,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Kinyua",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13202,
"legal_name": "John Kinyua Nderitu",
"slug": "john-kinyua-nderitu-2"
},
"content": "Asante sana, Bi. Spika wa Muda, kwa kunipa fursa hii. Kwanza kabisa, ningependa kuupongeza Mswada huu ulioletwa na Seneta Khaniri. Huu ni Mswada unaofaa Zaidi, kwa sababu askari wetu wamejitolea na kujizatiti kuilinda nchi yetu; kwa hivyo, familia zao zinafaa kulindwa ipasavyo. Hii ni kwa sababu hawa watu wamejitolea maisha yao ili kutulinda sisi na wengine, kwa hivyo ni vizuri Serikali na maofisa wanaohusika wachukue fursa ya kuangalia masilahi ya askari wetu, wanaofanya kazi nzuri sana. Hawa ni watu ambao wanajitolea maisha yao pamoja na familia zao na kuziweka katika hali ya tahadhari. Kwa hivyo, tuchukue fursa yoyote ambayo tunapata ili kuwasaidia. Bi. Spika wa Muda, najua kwamba kuna askari wengi waliopoteza maisha yao wakishughulikia nchi yetu. Familia zao hubaki katika hali hohe hahe, na wanashindwa kuelewa kwani nini hali imekuwa ngumu kwa kuwa familia iliyobakia haiangaliwi vizuri. Akina mama wanabaki wajane, watoto wanabaki mayatima na mtu mzee anabaki peke yake baada ya mke wake kupoteza maisha yake akiwa anashughulikia nchi hii. Unapata watu wanakosa motisha na uzalendo, kwa sababu hata wale waliokua na upendo kwa nchi yao, unapata hakuna mtu wa kuwashughulikia ipasavyo. Kwa hivyo, Bi. Spika wa Muda, naunga mkono Mswada huu, na kusema kwamba haifai watu hawa wachukuliwe kwa mzaha. Hawa ni watu ambao wamejitolea maisha yao, ambapo ni kinyume na, kwa mfano, mwalimu. Huyu ni mtu ambaye anabeba bunduki, na tunajua kwamba risasi ikitoka kwa bunduki, mpaka mtu afe ama ajeruhiwe. Nampongeza aliyeleta Mswada huu, kwa sababu wakati huu tunaoishi, kuna maafa mengi. Kwa mfano, kuna magaidi. Tunapata shida katika mipaka yetu kwa sababu The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate."
}