GET /api/v0.1/hansard/entries/961687/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 961687,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/961687/?format=api",
    "text_counter": 527,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Lungalunga, JP",
    "speaker_title": "Hon. Khatib Mwashetani",
    "speaker": {
        "id": 2163,
        "legal_name": "Khatib Abdallah Mwashetani",
        "slug": "khatib-abdallah-mwashetani"
    },
    "content": "Kama Mkenya, niko na imani Bw. Mbeo anaweza kufanya hii kazi. Kule kwangu Lungalunga, hivi tunavyozungumza tumeweza kuleta mwekezaji ambaye amejenga kiwanda kikubwa sana cha kusafisha samaki na kuwapeleka katika nchi za ng'ambo. Katika matarajio ambayo yatakuwa pale kwetu Lungalunga, sisi kama watu wa Kwale na lungalunga tutaweza kuajiri watu zaidi ya 3,000. Hiki kiwanda kimefika asilimia 100. Tunangojea halmashauri hii ambayo itachaguliwa kutupatia nafasi ya kuanza kusafisha wale samaki na kuendesha biashara. Kumekuwa na matatizo megi kuhusu mambo ya uvuvi kwa njia mbalimbali. Ukiangalia kanda ya kutoka Lamu mpaka Vanga, tuko na mipaka ambayo tunaruhusiwa kuvua na tuko na mipaka ambayo haturusiwi kuvua. Vilevile, matatizo mengine ni kuwa wakati mwingine, ukiangalia kwa upande wa bahari, wavuvi ambao wanatusaidia kutupa elimu ya kuvua ni wale wanaotoka Pemba. Kuna umuhimu wa kuwatambua kama Wakenya kwa sababu wengine wako katika maeneo ya Vanga, Jimbo, Jasini na Gazi. Hao wa Pemba wameingiliana na Wakenya kwani wameoana na kuzaana. Kwa hivyo, hii itakuwa nafasi moja ya kuelewa masuala ambayo yanatupa changamoto katika upande wa uvuvi. Tukiwa na mwenyekiti ambaye anafahamu masuala haya basi niko na imani ile halmashauri itaelekezwa kupeana msimamo kuhusu masuala kama haya."
}