GET /api/v0.1/hansard/entries/961688/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 961688,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/961688/?format=api",
    "text_counter": 528,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Lungalunga, JP",
    "speaker_title": "Hon. Khatib Mwashetani",
    "speaker": {
        "id": 2163,
        "legal_name": "Khatib Abdallah Mwashetani",
        "slug": "khatib-abdallah-mwashetani"
    },
    "content": "Jambo lingine ni kuwa juzi kama miezi miwili ambayo imepita, kulitoka maagizo kutoka Wizara ya uvuvi kuwa wavuvi wasitumie neti ndogondogo kuvua lakini kuna samaki kama bobwe, kule kwetu tunaita samaki bobe, ambao wanakua mpaka kiwango fulani na hawawezi kupita kiwango hicho. Hawa samaki ndio wanaotupa sisi kama wavuvi wa sehemu ya Kwale nguvu ya kuishi na kukimu maisha yetu. Sisi tunaomba Serikali ikubalie hizi neti zitumike kwa sababu ukivua samaki huwezi kupata samaki mwingine ambaye si ndugu wa samaki hao. Ni samaki ambao wanaishi kwa pamoja. Wanatembea pamoja na kila wakivuliwa utapata asilimia mbili peke yake pengine watakuwa samaki wadogo ambao Serikali inafikiri kuwa tunawamaliza kulingana na uvuvi wa namna ile. Kukiwa na halmashauri inayofahamu masuala kama hayo ikiongozwa na Mhe. Ochieng’ Mbeo ambaye pia namuunga mkono kuwa mmoja wa wale ambao watakuwa wanaendesha halmashauri hiyo, masuala kama hayo ambayo yanatupa changamoto katika sehemu zetu ambazo tunategemea uvuvi yataweza kurahisishwa. Ila tungeiomba Serikali pia iangalie haya masuala kwa sababu sasa hivi Blue Economy ni suala ambalo linaingia katika ulingo. Tunasema kwamba tuko tayari kama watu wa Lungalunga kushirikiana na mwenyekiti huyu ambaye ataingia ili tuweze kuboresha uvuvi katika maeneo tunayotoka."
}