GET /api/v0.1/hansard/entries/962024/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 962024,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/962024/?format=api",
    "text_counter": 251,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Faki",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13211,
        "legal_name": "Mohamed Faki Mwinyihaji",
        "slug": "mohamed-faki-mwinyihaji-2"
    },
    "content": "Asante sana, Bw. Naibu Spika kwa kunipa fursa hii ili niweze kuchangia Mswada huu wa Mgao wa Fedha mwaka wa 2019/2020. Mswada huu umekuja kwa wakati mwafaka kabisa. Tumeona kwamba hapo awali, kumekuwa na mtafaruku mkubwa katika serikali za kaunti kuhusiana na malipo ya malimbukizi ya madeni ambayo yanafuatana na kucheleweshwa kwa pesa hizi. Bw. Naibu Spika, ilikuwa ni makosa kwa Bunge la Kitaifa kutupilia mbali Mswada wa Seneti kwa sababu sisi sote ni Bunge moja. Ni majina tu mawili ambayo tumepewa kwamba, moja ni la Seneti na linguine ni la Kitaifa. Bunge hizi mbili zinapaswa kufanya kazi ambazo Katiba imewapa. Bw. Naibu Spika, Kifungu 218 cha Katiba kinasema kwamba, Mswada wa DORA ambao unahusu ugawaji wa pesa za kaunti unaweza kujadiliwa katika Bunge lolote; liwe la Seneti au lile la Kitaifa. Kwa hivyo, ilikuwa ni makosa kwa wenzetu wa Bunge la Kitaifa kutupilia mbali Mswada wetu. Hatufai kuwalaani kwa sababu tutakuwa tunajilaani wenyewe kama Bunge. Lakini sisi kama Bunge ambalo lina hadhi kubwa mbele ya macho ya wananchi, inatupasa kurekebisha matatizo ambayo yametokea. Bw. Naibu Spika, ningependa kuunga mkono mapendekezo ya kurejesha kiwango cha fedha kiwe Kshs335 billioni kama inavyopendekezwa katika Mswada huu. Ni kwa sababu kiwango hiki kimependekezwa na Kamati ya Ugavi wa Pesa za Serikali (CRA). Sisi kama Seneti tulikubaliana na mapendekezo yao kwa sababu Kamati hii ina mizizi yake katika Katiba yetu. Ni Kamati iliyoundwa kisheria. Hatuwezi kubadilisha mapendekezo yao bila ya kutoa hoja ambazo zinastahiki, kuonyesha kwamba tunaweza kubadilisha fedha zile. Bw. Naibu Spika, kwa hayo machache, ninaunga mkono Mswada huu."
}