GET /api/v0.1/hansard/entries/962598/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 962598,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/962598/?format=api",
"text_counter": 240,
"type": "speech",
"speaker_name": "Butere, ANC",
"speaker_title": "Hon. Nicholas Mwale",
"speaker": {
"id": 13311,
"legal_name": "Nicholas Scott Tindi Mwale",
"slug": "nicholas-scott-tindi-mwale"
},
"content": " Asante sana, Mhe. Naibu Spika wa Muda. Nimeona nichangie kwa lugha yetu ya kitaifa kwa sababu wenzangu wamechangia kwa lugha ya kimombo. Kila Mkenya anajua ya kwamba hili janga la ugonjwa wa saratani limetishia Wakenya wengi sana. Mhe. Naibu Spika wa Muda, naanza kwa kukwambia asante kwa kunipa fursa ya kuchangia Mswada ambao unahusu uchunguzi wa saratani ya kizazi. Kwanza, nataka kuwajulisha Wakenya kwamba ukiangalia utafiti uliofanywa na Serikali, utaona kwamba ugonjwa wa saratani ni ugonjwa wa tatu unaosababisha vifo vingi katika nchi yetu ya Kenya. Asilimia saba ya vifo nchini vinasababishwa na ugonjwa wa saratani. Nataka kuwajulisha Wakenya kwa jumla kwamba ugonjwa wa saratani unafaa upewe utafiti unaofaa, na pia Serikali inafaa izingatie kununua vifaa ambavyo vitawasaidia Wakenya haswa kwa kupimwa mapema ili wajue mbinu watakazotumia kutibu ugonjwa wa saratani. Nawaunga wenzangu mkono kwa kusema kwamba Serikali inafaa iongeze vifaa katika hospitali. Pia, Serikali inafaa izingatie kuwaelimisha Wakenya kuhusu ugonjwa wa saratani na kuwahamasisha kuhusu jinsi ya kuepuka ugonjwa huo, kama vile kutotumia vyakula ambavyo vinaleta dalili za ugonjwa wa saratani. Pia naihimiza Serikali ifanye uchunguzi na kuwaelimisha wananchi jinsi ya kuepuka ugonjwa wa saratani na pia njia mwafaka ambazo wanaweza kutumia kutibu ugonjwa wa saratani. Nakumbuka mwaka wa 1992, Serikali kuu ilisema kwamba ugonjwa wa malaria ni janga la kitaifa. Naiomba Serikali kuu ifanye vivyo hivyo. Tumefikia kiwango ambacho inafaa itangaze kwamba ugonjwa wa saratani ni janga la kitaifa ili kila Mkenya apate nafasi ya kuelimishwa, na hospitali zetu zipewe vifaa na wagonjwa wapewe matibabu ambayo yana technolojia ya juu zaidi ili Wakenya waishi bila uoga na pia tuone kwamba ugonjwa wa saratani hautasababisha vifo vingi katika nchi yetu ya Kenya. Kwa hivyo namshukuru Mhe. (Dkt.) Tecla Tum kwa kuleta Mswada huu ambao unaongea kuhusu saratani ya kizazi. Ninaonelea kwamba kwa vile ameleta saratani ya kizazi, tuchukue tu saratani kiujumla kwa sababu saratani katika nchi yetu ya Kenya iko na njia nyingi ambazo zinawadhuru wananchi. Kama tutasema tu twende na saratani ya kizazi peke yake, basi tutapoteza watu wengi ambao wanaugua saratani ambayo si ya kizazi. The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposes only. Acertified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}