GET /api/v0.1/hansard/entries/963131/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 963131,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/963131/?format=api",
"text_counter": 63,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Boy",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13200,
"legal_name": "Issa Juma Boy",
"slug": "issa-juma-boy"
},
"content": "Asante, Bw. Naibu Spika, kunipa fursa hii. Kwanza, ninamshukuru sana Sen. Halake kwa kuleta hii taarifa hii kwa sababu niliandamana na Maseneta wa Kamati ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia hadi Addis Ababa, Ethiopia. Nyumba na ofisi ya balozi wetu kule ni za aibu sana kwa Kenya. Taarifa hii imeletwa wakati mwafaka kwa sababu nilikuwa nasubiri iletwe ili niweze kuchangia. Ofisi za kule Addis Ababa ziko kwenye shamba la karibu ekari 11. Nyumba ambayo balozi wetu alikuwa anakaa ilikuwa karibu kuanguka. Tuliingia ndani na tukastaajabu. Wafanyakazi wa kule walituambia kuwa wamekuwa wakitoa malalamishi yao katika kila ofisi lakini hawajapata uzaidishi wowote. Kwa hivyo, naunga mkono taarifa hii iliyoletwa na Sen. Halake. Kamati itakayoshughulikia taarifa hii inafaa kwenda Addis Ababa, Ethiopia, ili wajionee wenyewe. Huo si uwongo bali ni aibu."
}