GET /api/v0.1/hansard/entries/963155/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 963155,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/963155/?format=api",
    "text_counter": 87,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Faki",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13211,
        "legal_name": "Mohamed Faki Mwinyihaji",
        "slug": "mohamed-faki-mwinyihaji-2"
    },
    "content": "(1) Hatua ya Mamlaka ya Kitaifa ya Bandari (KPA), Shirika la Kitaifa la Reli na Mamlaka ya Ukusanyaji Ushuru kuhamisha utoaji wa vibali yaani clearance certificates za mizigo kutoka Bandari ya Mombasa hadi sehemu nyingine za nchi na nchi jirani. (2) Iwapo Serikali imetathmini athari ya kuhamisha utoaji wa vibali hivyo vya kusafirisha mizigo hadi Nairobi kwa uchumi wa Kaunti ya Mombasa na kaunti jirani. (3) Kueleza ni mikakati gani iliyowekwa na Serikali kutoa ajira mbadala kwa watakaoathiriwa, hasa watakaopoteza ajira au namna ya kuvumbua riziki. (4) Kueleza iwapo sera ya soko huru katika biashara imetupiliwa mbali na hasa shinikizo kutoka kwa Serikali kwamba wafanyibiashara wanapaswa kusafirisha shehena zao kwa kutumia reli. (5) Iwapo hatua hiyo ya kuhamisha kituo cha kutoa vibali vya kusafirisha mizigo kutoka Bandari ya Mombasa inaweza kusimamishwa ili kutoa nafasi ya watu kushauriana kuhusiana na swala hilo. Asante, Bw. Naibu Spika."
}