GET /api/v0.1/hansard/entries/963291/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 963291,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/963291/?format=api",
    "text_counter": 223,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Faki",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13211,
        "legal_name": "Mohamed Faki Mwinyihaji",
        "slug": "mohamed-faki-mwinyihaji-2"
    },
    "content": "ambayo imewekwa katika kifungu cha sita, wote ni wafanyikazi wa kaunti. Kwa hivyo, ni rahisi kwao kuhakikisha ya kwamba mawazo ya gavana yanatekelezwa kwa sababu wote ni wafanyakazi wa serikali za kaunti. Hivyo basi wote wana allegiance ya karibu kwa gavana. Kwa hivyo hawawezi kupinga maamuzi yake. Ningependekeza hapa ya kwamba kamati hiyo iwe na watu zaidi kutoka nje, yaani wakaazi wa kaunti ile ambao hawahusiani na serikali ya kaunti kwa jambo lolote la kikazi ama kibiashara. Hii itaipa kamati ile uhuru wa kufanya mambo wanayotaka bila kushurutishwa na sehemu yeyote. Ningependekeza pia kwamba kati ya wale ambao watakaa katika kamati hii, wawe wamehusika michezoni kwa muda mrefu na vile vile wafanyikazi wastaafu katika nyanja mbalimbali za kibiashara. Hii itasaidia pakubwa kuleta usawa na haki katika maamuzi ya kamati hiyo. Hii ni kwa sababu kamati hii ni muhimu kabisa katika kuamua ni nani anastahili kupewa fursa ya kuwa katika ukumbi wa umaarufu. Bi. Spika wa Muda, tumeona pia ya kwamba katika Mswada huu gavana anapewa fursa ya kufutilia mbali mtu yeyote ambaye amepewa tuzo kama hiyo kwa sababu ya vigezo fulani. Ingekuwa bora kama sababu ambazo zinaweza kutumika kumpokonya mtu aliyepewa tuzo ziweze kutajwa hapa ili kusiwe na tashwishi kwamba haki imepatikana, wakati mtu amepokonywa ama amefutiliwa mbali ile tuzo ambayo amepewa Bi. Spika wa muda, tukiiwacha wazi, sababu nyingi zinaweza kutumika kumpokonya mtu tuzo, kwa mfano mtu akipinga maamuzi fulani ya serikali ya kaunti na mengineyo. Inahakikisha kwamba mtu hapewi fursa ya kujitetea kabla ya kupokonywa tuzo ambayo amepewa. Katika nyanja za michezo, wachezaji wengi wa taifa letu wanaishi katika hali ngumu hivi sasa. Ametajwa hapa mwanadada bondia Conjestina Achieng’ ambaye alileta ufahari mkubwa na kuwatia motisha wasichana wengi kushiriki michezo . Mchezo ule mara nyingi unahusishwa na vijana wa kiume. Lakini, alitia motisha wengine wakaweza kushiriki mchezo ule na kwa sasa hali yake ya kiafya na kimaisha si nzuri. Hii ni kwa sababu hana kazi ama njia yoyote ya kuweza kupata pesa. Ninafurahia kwamba serikali ya Kaunti ya Kisii imewatambua baadhi ya wachezaji wa zamani akiwemo Henry Motego ambaye ameajiriwa kama afisa wa michezo. Hapa Nairobi pia tunaona kwamba George Sunguti ameajiriwa kama afisa wa michezo kusaidia kuimarisha michezo katika kaunti. Bi. Spika wa Muda, Mswada huu utasaidia pakubwa kuweza kutambua watu ambao wamebobea katika fani mbali mbali katika kaunti zetu na vile vile kuwatuza. Pia kutakuwa na vigezo fulani ambavyo vinaweza kutumika kutoa tuzo zile. Tuzo haizifai kutolewa kiholela, kwa mfano kuwapa wafuasi wa karibu wa gavana. Hiyo itakuwa The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate."
}