GET /api/v0.1/hansard/entries/963515/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 963515,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/963515/?format=api",
"text_counter": 142,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Zawadi",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13176,
"legal_name": "Christine Zawadi Gona",
"slug": "christine-zawadi-gona"
},
"content": "Ahsante Mheshimiwa Spika kwa kunipa nafasi hii ili nitoe maoni yangu kuhusu Taarifa iliyo letwa na Seneta wa Tana River. Naunga mkono yale ambayo yamesemwa. Vile vile, ninashangaa. Mvua inafaa kuwa baraka kwa watu wetu lakini kuna wakati ambapo huwa haikuwi baraka bali inaleta maafa na laana kwa watu. Mvua hainyeshi kwa bahati mbaya. Tunajua ya kwamba tuko na msimu wa mvua na msimu wa kiangazi. Ninashangaa ni kwa nini hakuna viegezo vinawekwa ili kuzuia maafa wakati wa mvua. Nasema hivyo kwa sababu tunaishi nyanda za chini, na hata sio sisi peke yetu, kuna Wakenya wengi kule. Mvua inaponyesha, mvua iliyonyesha nyanda za juu huteremka kwetu. Kwa hivyo, vifo vingi hutokea kwa sababu mvua inaponyesha, ajabu ni kwamba maji haya hayafiki mapema ili watu wajipange. Mara nyingi maji hufika usiku wakati watu wamelala. Hua ninashangaa kuhusu kina mama na watoto, kwa sababu mara nyingi vifo huwapata kwa sababu huwa wamelala wakati huo. Afadhali wazee hua bado wako nje,"
}