GET /api/v0.1/hansard/entries/963517/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 963517,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/963517/?format=api",
    "text_counter": 144,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Zawadi",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13176,
        "legal_name": "Christine Zawadi Gona",
        "slug": "christine-zawadi-gona"
    },
    "content": "lakini akina mama na watoto hupatwa wakiwa ndani wamelala. Tumepoteza akina mama na watoto wengi kwa ajili ya mvuo hiyo. Jambo hili si la jana, leo, wala la juzi; limekupwepo tangu jadi. Ninashangaa ni kwa nini Serikali haingalii namna ya kuokoa maisha. Kwani kila siku tutakua tunakimbia kuwapelekea tents na mabati? Tutafute njia mbadala ya kuhakikisha kwamba, watu hawatapoteza maisha tena. Mvua hii inaponyesha, kuwe na viegezo vitakavyokua vinawekwa, kama kuchimba dams ili maji haya yasipotelee bahari kavu. Tunaviojua, hakuna maji haswa katika sehemu za wafugaji, ilhali mvua inanyesha. Kwa nini hizo dams hazichimbwi sasa ili mvua inaponyesha, kuingie maji ili ng’ombe na mbuzi wao wapate malisho, na pia kuyatumia maji kulima kwa wale ambao ni wakulima? Sisi tumekua tukiwacha maji hayo yaende baharini. Ninafikiri imefika wakati sasa. Mjadala huu sijaskia kwa mara ya kwanza au wa pili; umekuwa ukirudiwa rudiwa, lakini bado hakuna hatua ambazo zimechukuliwa. Kwa sasa, mvua bado inaendelea. Wakati umefika wa kuchukulia watu wetu umuhimu mkumbwa. Kabla ya mambo mengine, tuangalie maisha ya wanadamu na mifugo. Mtu anaweza lala tajiri na amke maskini akiwa sehemu hizo. Hii ni kwa sababu maji yakija usiku; yabebe ngombe wako wote, chakula chako kwa shamba na watoto. Unalala ukiwa na mali na unaamka ukiwa maskini kwa ajili ya maji ambayo yanapaswa kuwa faida kwa wananchi. Nimesisama kuunga mkono watu wa Tana River kwa sababu mimi ninatoka Kilifi, na hali ni hiyo hiyo. Ukienda sehemu za Sabaki, utakuta hali ni hiyo hiyo; maji huja na kusomba watu. Wakati umefika ambapo inafaa majanga haya yote yaishe na tutafute njia ambayo itasaidia watu wetu."
}