GET /api/v0.1/hansard/entries/964579/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 964579,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/964579/?format=api",
"text_counter": 377,
"type": "speech",
"speaker_name": "Wundanyi, WDM-K",
"speaker_title": "Hon. Danson Mwashako",
"speaker": {
"id": 13509,
"legal_name": "Danson Mwashako Mwakuwona",
"slug": "danson-mwashako-mwakuwona"
},
"content": " Asante, Mhe. Naibu Spika. Wakati Mhe. Millie Odhiambo alipokuwa akiitisha hoja ya nidhamu, tulingoja tusikie ni gani. Leo ametaja chura kwamba wengine ni wanadamu lakini wengine ni chura. Sikuelewa ilitokea wapi lakini tunamuelewa maana yeye ni gwiji katika mambo ya Bunge. Ninasimama kuunga mkono mjadala huu ambao umeletwa ndani ya Bunge kuongea masuala ambayo yamekumba nchi yetu haswa masuala ambayo yanafungamana na lile janga ambalo limetokea kule West Pokot, kaunti ambayo Mhe. Moroto anatoka. Nampongeza sana. Kama mzee na mheshimiwa wa Bunge hili, ameleta jambo hili ambalo limeangaziwa sana katika vyombo vya habari. Bunge la Taifa limepata nafasi nzuri ya kujadili suala hili. Kwa kweli, janga hili ni zito. Ni janga ambalo Kenya nzima imepigwa na butwaa. Tunapoangalia runinga, tunaona watu wa huko wanateseka. Kwa niaba ya watu wangu kutoka Wundanyi na Taita Taveta, natoa pole zangu kwa Mhe. Moroto na Wabunge wote wa maeneo ya West Pokot na kuwapa pole. Munge akaweke roho za wale waliopoteza maisha yao mahali pema peponi. Pia nachukua nafasi hii kueleza Bunge hili na nchi nzima kwamba janga hilo halikutokea West Pokot peke yake. Mambo haya yametendeka kaunti nyingi nchini na kaunti yangu ya Taita Taveta imekuwa pia mojawapo ya kaunti ambazo zimepigwa sana na mambo haya. Kweli, tulilia mvua na tukatamani sana mvua inyeshe lakini mvua ya mwaka huu hatujaiona miaka mingi. The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposes only. Acertified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}