GET /api/v0.1/hansard/entries/964580/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 964580,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/964580/?format=api",
    "text_counter": 378,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Wundanyi, WDM-K",
    "speaker_title": "Hon. Danson Mwashako",
    "speaker": {
        "id": 13509,
        "legal_name": "Danson Mwashako Mwakuwona",
        "slug": "danson-mwashako-mwakuwona"
    },
    "content": "Mimi ambaye ninatoka maeneo yale ya miinuko kama kule Taita na Wundanyi, tumepata taabu kubwa. Kule kwangu, juzi tulipoteza mtoto mdogo ambaye nyumba yao ilisukumwa na maporomoko ya ardhi. Leo hii, tunavyoongea hapa, mchana wa leo, kulikuwa na kamati ya kushughulikia majanga kule kwangu Wundanyi ikiongozwa na mkuu wa kata ndogo ya Wundanyi, Taita, wakitathmini hasara iliyoletwa na maporomoko yale. Mhe. Naibu Spika, naomba kukujuza. Asilimia 60 ya Eneo Bunge langu la Wundanyi ni miinuko ambayo wakati mvua ilipoanza kunyesha, leo hii nina familia 170 ambazo zimeathirika sana na masuala haya. Nashukuru juzi niliongea na Waziri Matiangi na kumjulisha kwamba kule kwangu nina matatizo makubwa. Nashukuru kwa sababu alituma msaada kupitia afisi ya mkuu wa R egional Commissioner kule Mombasa wakaongea na C ounty Commissioner wakatathmini hasara iliyoletwa na maporomoko yale. Familia 170 ziliathirika na kila familia ina watu karibu sita. Zingine zina watu saba na nane. Kwa hivyo, nina watu elfu moja ambao wameathirika sana kutokana na maporomoko yale. Alafu tena nyumba zao zote zimebomolewa. Ni jambo ambalo Bunge hili najua tuko na mfuko, bajeti na leto tumeweka budget estimates za S upplementaryBudget . Tuna pesa inayoitwa Disaster Management Fund. Naomba kwamba watu wale wakapewe fidia. Ikiwezekana nyumba zile zikajengwe tena na Serikali maana watu wale hawana mbele wala nyuma. Ni watu maskini. Pesa za kukula na kusomesha watoto wao ni shida. Leo hii, hawana makao. Naomba Bunge hili, wakati linapomaliza mjadala huu, liseme kwamba Serikali ya kitaifa inapoendelea kujengea watu walioathirika kule West Pokot nyumba, kule Taita Taveta na Wundanyi pia wajengewe nyumba. Nashukuru Red Cross na World Vision wamesema kesho kutwa wanapeleka mablanketi na neti za mbu ili tuwasaidie watu wetu. Serikali lazima ikafidie watu wale na wakajengewe nyuma ili wakarudishwe katika hali walizokuwa mbeleni. Vile vile, barabara zimeathirika sana. Tunaomba kwamba Serikali, kupitia KeRRA, itume pesa kule mashinani ili West Pokot, Taita, Isiolo na Tana River ambako kuna shida barabara zikarudishwe katika hali zilizokuwa. Namalizia hapo kwa sababu muda wangu umeisha lakini hili ni jambo ambalo Serikali lazima iangalie."
}