GET /api/v0.1/hansard/entries/964654/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 964654,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/964654/?format=api",
"text_counter": 452,
"type": "speech",
"speaker_name": "Tana River CWR, MCCP",
"speaker_title": "Hon. (Ms.) Rehema Hassan",
"speaker": {
"id": 13275,
"legal_name": "Rehema Hassan",
"slug": "rehema-hassan"
},
"content": "Pia, ningependa kuongeza sauti wakati jambo kama hili la huzuni limetokezea na kuwaomba Waheshimiwa wenzangu tusiwakejeli wenzetu. Wakati wenzetu wamepoteza watu wao na wanahuzunika, sisi huku tunakuja kulifanya jambo la siasa hapa. Wengine bado hawajapata watu wao, wala kuwazika na sisi hapa tunafanya siasa nyingi badala ya kutafuta suluhu ya kudumu ya hiyo shida. Mimi pia watu wangu wa Tana River tunavyozungumza, kuanzia hapa Ziwani karibu na Garissa na Garseni sehemu ya Tana Delta, watu wamepoteza makaazi, mimea na hata mifugo yao. Hawana mahali pa kulala. Mimi pia ningeomba Serikali iwasaidie. Ile idara ambayo iko kwa kaunti hata kwa Serikali bado ipo."
}