GET /api/v0.1/hansard/entries/965192/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 965192,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/965192/?format=api",
    "text_counter": 113,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Boy",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13200,
        "legal_name": "Issa Juma Boy",
        "slug": "issa-juma-boy"
    },
    "content": "ambayo imeletwa hapa na Sen. Mwaruma kutoka Kaunti ya Taita-Taveta. Kusema kweli, hata Kaunti yangu ya Kwale ina shida kama hiyo. Baada ya utalii, mapata mengine yanatokana na madini. Sisi tuna madini ambayo yanaitwa Titanium . Tangu Base Titanium Company ianze kuchimba madini, wananchi wa Kwale hawajafaidika kupata haki yao mpaka sasa. Bw. Spika, kusema kweli, kampuni zinazochimba madini zinapata mabilioni ya pesa lakini wananchi ambao ardhi zao zimenyakuliwa hawapati chochote. Hizi kampuni huwadanganya kuwa watawajengea hospitali na mabweni ya shule lakini mwananchi hafaidiki na chochote kutokana na biashara hiyo. Bw. Spika, naunga mkono hii Statement kwa sababa inagusia kilio kikubwa cha watu wa Kaunti ya Kwale. Lengo la kufanya hivyo ni kuhakikisha kuwa wananchi wa Kwale na kaunti zingine wanapata haki. Kwa hivyo, ningependa kuhimiza Kamati na Wizara ambazo zitachunguza jambo hili kutafuta njia ya kuhakikisha kwamba wananchi wa Kenya wanapata haki. Hatutaki kuona wenye makampuni wakifaidika kwa kupata mabilioni na kupeleka pesa zao Ulaya ilhali wananchi wetu wanateseka."
}