GET /api/v0.1/hansard/entries/965195/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 965195,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/965195/?format=api",
    "text_counter": 116,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Wario",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13224,
        "legal_name": "Golich Juma Wario",
        "slug": "golich-juma-wario"
    },
    "content": "Kaunti zote za pwani ziko na mali asili na watu wa pwani wanaweza kufaidika na hiyo mali. Mimi ninatoka Kaunti ya Tana River na tuko na madini ambayo inaweza kufaidi watu wa Tana River. Sheria na kanuni za kuchimba madini hazifuatwi. Kuna shimo kubwa ambazo zimebaki katika zile sehemu ambapo gypsum ilitolewa na ingekuwa vyema kama miti ingepandwa katika hizo sehemu. Hizo shimo zinasababisha maafa ya ng’ombe, mbuzi na hata wanadamu. Badala ya kuleta usaidizi kwa wenyeji, hayo madini yamekuwa hatari kwao. Ninaunga mkono hii Taarifa. Serikali za kaunti na Serikali kuu zinafaa kusaidia wenyeji ili waweze kufaidika na madini ambayo yanapatikana kwao. Hiyo itatuwezesha kutoa umaskini ambao uko sehemu hizo."
}