GET /api/v0.1/hansard/entries/965201/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 965201,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/965201/?format=api",
"text_counter": 122,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Madzayo",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 679,
"legal_name": "Stewart Mwachiru Shadrack Madzayo",
"slug": "stewart-mwachiru-shadrack-madzayo"
},
"content": "Asante, Bw. Spika, kwa kunipa nafasi hii ili niweze kuweka mkazo kwa Taarifa hii iliyoletwa na ndugu yetu Seneta wa Taita-Taveta. Katika miaka 40 iliyopita, kama kulikua na mji maskini, ulikua mji wa Dubai. Kule nyumbani tunauita Dubai. Dubai ilikua mji maskini sana; watu walikua wanatamebea na ngamia, kama vile kule North Eatsern. Lakini, leo Dubai inaheshimiwa duniani nzima na kila mtu angetaka kuenda huko, kwa sababu wameinua uchumi wao hali kwamba, hawajivunii rasilmali ya petroli peke, bali pia utalii. Bw. Spika, nchi yetu imebarikiwa sana. Kule upande wa Turkana, kuna petrol, na kule Migori, kuna dhahabu. Ukienda Pwani, kuna titanium, na nyinginezo. Nchi yetu imebarikiwa sana, lakini kwa sababu ya tamaa ya watu binasfi, tumepoteza nafasi hio. Miaka iliyopita, wakati Rais Kenyatta alikua anatawala nchi hii, alisema watu wa Taita - na sisemi hivyo kwa sababu ndugu yangu yuko hapa, lakini yeye aliongelewa na aliyekua Rais wetu wa kwanza. Alisema kwamba tumekalia uchumi, na sijui kama hio ndio sababu shamba zao na milima zao zilichukuliwa. Jambo la kusikitisha ni kwamba, ufisadi nchini humu umefanya hatuwezi kupata rasilimali zetu. Kama vile Seneta wa Nairobi alivyosema, mahali ambapo malalamishi yanapatikana kwa wingi Kenya nzima, ni Kilifi. Hii ndio sababu barabara zimegeuka rangi. Inakua rangi ya ile mchanga. Ikiwa Taarifa kama hii itaenda kwa Kamati Chunguzi ya Madini, itaweza kuchunguza vizuri sana na kuchukua hatua ya kumuuliza Waziri amefanyia nini vitengo vyote, na tuweze kujua jawabu lake kwa umakini. Ninaunga mkono Taarifa hii na kumshukuru ndugu yangu kwa kuileta Bungeni."
}