GET /api/v0.1/hansard/entries/966517/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 966517,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/966517/?format=api",
    "text_counter": 16,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Madzayo",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 679,
        "legal_name": "Stewart Mwachiru Shadrack Madzayo",
        "slug": "stewart-mwachiru-shadrack-madzayo"
    },
    "content": "Bw. Spika, kitu muhimu ambacho nawaeleza ndugu zangu, wakiwa hapa ni kwamba, ile Ripoti ya Building Bridges Initiative (BBI) ikija kwao, inatakikana kila mtu apate nafasi aipitie, aisome na aielewe. Ikiwa kuna vipengele fulani ambavyo mngependelea pengine virekebishwe ama muweze kuweka kanuni zenu pale ndani, ili kanuni zenu ziweze kusiskika, tuko na “baba” yetu hapa, Mhe. Haji, ambaye ni Seneta na Mwenyekiti wa hiyo Tume ya BBI. Bw. Spika, nakushukuru sana kwa makaribisho hayo. Natumai kwamba watu wa Kilifi wamefurahi sana. Kumalizia, tutakapochukua Seneti Mashinani mwaka ujao, watu wa Kilifi wameniambia ya kwamba nikuombe kwamba Seneti Mashinani mwaka ujao iwe ndani ya Kaunti ya Kilifi. Asante, Bw. Spika."
}