GET /api/v0.1/hansard/entries/966607/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 966607,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/966607/?format=api",
    "text_counter": 106,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Madzayo",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 679,
        "legal_name": "Stewart Mwachiru Shadrack Madzayo",
        "slug": "stewart-mwachiru-shadrack-madzayo"
    },
    "content": "Kwa hivyo, mimi ninataka kujuwa ni lini; hasa kile kipande cha kuanzia pale Mtwapa mpaka kule mwisho wa weigh bridge; ni kipande cha mita 300. Utashangaa kwa sababu inachukuwa masaa mawili, mawili na nusu au matatu kuvuka pale katikati. Unaweza kutafakari kwamba, masaa matatu ama mawili na nusu kupita kiwango cha mita 300 pekee yake. Hiyo imeleta shida kubwa sana. Hata afadhali ingewachwa vile ilivyokuwa kuliko kuiharibu mkisema kwamba mtatengeneza halafu haitengenezwi. Hilo ni swala ambalo nilikuwa ninataka liwekwe kupaumbele. Bw. Spika jambo la mwisho ni, ile barabara ya kutoka Kilifi hadi Bamba. Mheshimwa Rais alikuja akasema ya kwamba hii barabara ya kutoka Kilifi mpaka Bamba itafanywa na hata akaimba nyimbo kwamba safari ya bamba ni machero. Aliimba nyimbo ya kigiriama hata mimi nikashangaa. Lakini ninataka kuuliza; tangu Rais aseme hivyo, wale watu wanambwaga Rais ni wale watu ambaao wanamfanyia kazi; mawaziri wake. Kwa hivyo, mimi ninataka mwenyekiti wa mambo ya barabara ndani ya Seneti aweze pia kunakili na kujuwa hii barabara ya kutoka Kilifi mpaka Bamba itaanzishwa lini na itamalizwa lini, kadri ya vile Rais wa Jamhuri ya Kenya alivyoamrisha. Asante sana."
}