GET /api/v0.1/hansard/entries/968012/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 968012,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/968012/?format=api",
    "text_counter": 41,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Kinyua",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13202,
        "legal_name": "John Kinyua Nderitu",
        "slug": "john-kinyua-nderitu-2"
    },
    "content": "Asante sana, Bw. Spika, kwa kunipa fursa hii. Naunga mkono Ombi hili. Hili ni jambo ambalo limekuwa la kawaida, kwa watu kutimuliwa bila kufuata mikakati mizuri. Unapata kwamba ukitembea katika sehemu za nchi ukienda Mlimani Marmanet na Sori, watu wanafukuzwa na wamepelekwa huko, lakini unapata hakuna shule ama hosipitali. Watu wanaishi maisha ya ufukara, na ni aibu, kwa sababu Serikali inafaa iwe na mikakati iliyowekwa vizuri. Kabla mtu yeyote hajafukuzwa, lazima mambo ya shamba yafuatwe, na mahali wale watu watakapopelekwa ijulikane ni wapi. Baada ya hiyo, wanaondolewa wakizingatia kanuni za kibanadamu, badala ya kuwafurusha watu kama wanyama. Serikali yoyote inapotengenezwa, jukumu lake kubwa huwa ni kutunza na kulinda mali pamoja na uhai wa binadamu. Lakini inapokuwa kazi ya Serikali ni kuwafurusha watu kiholela, inaonekana kana kwamba hawana faida yoyote kwa wananchi. Kwa hivyo, Bw. Spika, ningeomba kwamba Kamati itakayopewa jukumu hilo wanzingatie na waambie maafisa wanaohusika wafuatilie mikakati ambayo itakuwa inazingatia manufaa ya watu. Kama ni kufukuzwa, basi wawe wakiulizwa na wanapelekwa mahali ambapo patawafaa. Asante, Bw. Spika."
}