GET /api/v0.1/hansard/entries/968905/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 968905,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/968905/?format=api",
    "text_counter": 451,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Mvita, ODM",
    "speaker_title": "Hon. Abdullswamad Nassir",
    "speaker": {
        "id": 2433,
        "legal_name": "Abdulswamad Sheriff Nassir",
        "slug": "abdulswamad-sheriff-nassir"
    },
    "content": "Takriban siku tatu or nne zilizopita, kwa sababu ya milango kutofanya kazi, mtu mmoja kwa sababu ya mvua, aliteleza na kuingia ndani ya maji. Lau angelikuwa mjasiri na kama hakungekuwa na boti ya haraka, leo tungekuwa tunazungumza masuala mengine. Kenya haitasahau tarehe 29 September 2019. Wakenya wawili, mama na mwanawe, walipoteza maisha yao. Ninapongeza wanakamati wenzangu kwa kazi waliofanya. Naipongeza afisi ya Karani Mkuu wa Bunge na pia afisi ya Spika kwa usaidizi wa kuhakikisha kuwa tumeandaa Ripoti hii."
}