GET /api/v0.1/hansard/entries/968909/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 968909,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/968909/?format=api",
"text_counter": 455,
"type": "speech",
"speaker_name": "Mvita, ODM",
"speaker_title": "Hon. Abdullswamad Nassir",
"speaker": {
"id": 2433,
"legal_name": "Abdulswamad Sheriff Nassir",
"slug": "abdulswamad-sheriff-nassir"
},
"content": "Tatu, tunataka Serikali kupitia kwa Wizara ya Fedha, itoe pesa kwa KFS. Tulipokuwa tunafanya Ripoti hii, ilisemekana kuwa fedha zinatoka lakini baada ya ile siku tulikuwa tunaandika Ripoti, fedha hazikuwa zimefika kwa KFS. Kwa hivyo, tunashurutisha Serikali itoe fedha za kuhakikisha kuwa marekebisho yamefanyika. Pia, hizi fedha ziziregeshwe tena katika Serikali Kuu mwisho wa mwaka bali zibaki ili zitumike kutengeneza feri. Kwa lugha ya kitaaluma ya Bunge na sheria, zile fedha ziwe ring-fenced . Pili, afisi ya Mkaguzi Mkuu iangalie ule mkataba uliopo baina ya kampuni ya African Marine and General Engineering na KFS kwa sababu hiyo ndio kampuni pekee ambayo inaweza kufanya utengenezaji wa feri kwa kitanda cha chini. Tunataka afisi ya Mkaguzi Mkuu iangalie kwamba fedha zinatumika ifaavyo. Tunasema shirika la Kenya Ports Authority pia liangalie uwezekano wa kuhakikisha ya kuwa wameweka sehemu ya kutengeza hizi feri ili gharama hizi zipungue. Tunataka Kenya Maritime Authority waangalie wanayozungumza kwa sababu, bila shaka, ni urongo walipeana kwa Kamati kuwa walikagua hizi feri. Hawakuzikagua. Tunataka pia, kwa kuwa tumegundua Kenya Maritime Authority, wale walipewa kazi ile ya ukaguzi wana miaka 70 na zaidi. Ni watu wawili pekee. Suala ni kuwa hawa wasipokuwa, vifaa vyote vitakaguliwa na nani? Tutaka Serikali ikiweka bodi za Kenya Ferry Services, isitafute watu ambao hawana taaluma yoyote. Watafute watu ambao wana taaluma ya ubaharia."
}