GET /api/v0.1/hansard/entries/968911/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 968911,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/968911/?format=api",
"text_counter": 457,
"type": "speech",
"speaker_name": "Mvita, ODM",
"speaker_title": "Hon. Abdullswamad Nassir",
"speaker": {
"id": 2433,
"legal_name": "Abdulswamad Sheriff Nassir",
"slug": "abdulswamad-sheriff-nassir"
},
"content": "Watafute watu walio na taaluma ya kazi za uinjinia. Watafute watu wenye taaluma kadha wa kadha. Tunasema kuwa Kenya Maritime Authority wahakikishe kuwa wanaajiri wafanyakazi. Wanakusanya Kshs1.2 bilioni kwa mwaka. Waajiri wale wa kuzama chini kwa chini na wale wa kuzama ndani ya maji ili kuhakikisha usalama wa zile feri. Wakati hauko nasi. Nitawacha hizi zingine. Ninajua ni jambo la uchungu kwa wale wanaotumia feri hizi zikizuiliwa. Serikali haitoweza kusikia mlio wa watu isipokuwa panapokuwa na tatizo. Hatuwezi kukubai hili tatizo. Ni afadhali tuwe na tatizo la watu kuzuiwa vivukio kidogo kuliko tatizo la vifo kwa jambo linaloweza kurekebishwa kwa miezi. Asante sana Naibu Spika wa Muda. Naomba Naibu Mwenyekiti wangu aniunge mkono katika jambo hili."
}